MAPINDUZI CUP 2019 | YANGA SI LOLOTE KWA AZAM FC | Yanga 0-3 Azam FC

Category: 

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imefanya kweli baada ya kuichapa Yanga mabao 3-0 kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi uliomalizika leo Jumamosi usiku.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kupanda kileleni mwa msimamo wa Kundi B ikiwa na pointi nne sawa na Malindi lakini matajiri hao wakiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na Obrey Chirwa aliyefunga mawili na Enock Atta, akifunga jingine kwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja nje kidogo ya eneo la 18. #MapinduziCup2019 #TimuBoraBidhaaBora #AfricanFrutiImenogaFresh
#UhaiDrinkingWater #TradegentsTanzaniaLimited

Back to Top